Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Dr Wilbroad Slaa
anatarajiwa kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara Mjni Same siku ya
Jumanne Januari 15, 2013.
Kwa mujibu wa maelezo ya Mratibu Mkuu
wa mkutano huo mkubwa, Bw Christopher Mbajo, Dr Slaa anatarajiwa pia
kuzindua Ofisi ya CHADEMA Kata ya Hedaru na kufungua matawi ya chama
hicho katika maeneo ya Hedaru, Makanya na Same.
Akifafanua zaidi, Bw Mbajo anaeleza kuwa maandalizi yote ya mkutano huo
yanakwenda vizuri na kuwataka wananchi wali karibu na maeneo hayo
kujitokeza kwa wingi siku hiyo kusikiliza kile ambacho Katibu Mkuu huyo
atawaambia.
Katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kilichoketi
Disemba 15-16 mwaka jana, chama hicho kiliazimia kwamba mwaka huu wa
2013 utakuwa ni mwaka wa kuunganisha nguvu ya umma kitaifa, kuishinikiza
serikali ya Rais Jakaya Kikwete kutoa tamko juu ya kuundwa tume huru ya
kimahakama, itakayochunguza ya mauaji mbalimbali ya utatanishi
yaliyotokea nchini katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Mbali na kuunganisha nguvu ya umma, chama hicho pia kiliazimia kuitumia
kambi rasmi ya upinzani bungeni kutumia njia za Kibunge kupitia hoja
binafsi au muswada binafsi kuwasilisha bungeni mapendekezo ya
marekebisho ya Katiba ya mpito kuhakikisha Tume Huru ya Uchaguzi na
marekebisho ya sheria zinazosimamia uchaguzi, yanafanyika kabla ya
Katiba Mpya.
Posted in:
0 comments:
Post a Comment